Kijana akijaribu bahati yake mbele ya Majaji Salama, Madame Ritha na Master J.
Majaji Salama, Madam Ritha na Master J wakiwasikiliza washiriki waliojitokezano kujaribu bahati yao katika kutafuta washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search.
Baadhi ya washiriki wakisubiri kuingia ndani ili kujaribu bahati yao mbele ya Majaji
ZAIDI ya vijana 5,000 wamejitokeza
katika usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star
Search katika fukwe za Coco leo.
Usaili huo ambao utakuwa ni wa siku tatu umeonekana kuwa ni wa aina
yake hasa kutokana na idadi kubwa ya vijana waliojitokeza jana ikiwa
ndio siku ya kwanza.
Katika sehemu mbalimbali za uwanja huo ilionekana kujazwa na vijana hao
ambao wengi wao walikuwa wakiimba huku wengine wakiwa wanafanya
mazoezi ya kutumia aina mbalimbali za vifaa vya muziki.
Akizungumzia shindano hilo, jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen
alisema kuwa Dar es Salaam ambao ndio mkoa wa mwisho katika usaili huo
hamasa imekuwa kubwa sana kwa washiriki huku wengi wao wakiwa na
matumaini makubwa ya kuchaguliwa.
"Tumeona vijana wazuri sana, na kama kawaida ya Dar tunatarajia
ushindani mkali kwa mkoa huu, na ndio maana tutachukua vijana kumi na
saba kutoka hapa," alisema Ritha.
Afisa Biashara wa Zantel, Sajid Khan, amepongeza umati mkubwa wa watu
uliojitokeza kwa upande wa Dar es Salaam akisema kwa vipaji
vilivyopatikana mwaka huu watu watarajie burudani ya kutosha vipindi
vikianza kuonyeshwa kwenye luninga.
"Tunatoa zawadi kubwa kwa mwaka huu, Sh. milioni 50 pamoja na mkataba
wa kurekodi, hivyo vijana wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi
kutimiza ndoto zao," alisema Khan.
Zoezi hili litaendelea siku ya kesho (Alhamisi) na kesho (Ijumaa)
ambapo washiriki 17 watakaopatikana wataungana na wengine 33 kutoka
mikoani kufikisha idadi ya washiriki hamsini watakaoingia kambini.
No comments:
Post a Comment